Sababu 05 Zinazofanya Watu Wakudharau...!
M4A•Źródło odcinka
Manage episode 382910166 series 3280689
Treść dostarczona przez Innocent Ngaoh. Cała zawartość podcastów, w tym odcinki, grafika i opisy podcastów, jest przesyłana i udostępniana bezpośrednio przez Innocent Ngaoh lub jego partnera na platformie podcastów. Jeśli uważasz, że ktoś wykorzystuje Twoje dzieło chronione prawem autorskim bez Twojej zgody, możesz postępować zgodnie z procedurą opisaną tutaj https://pl.player.fm/legal.
Hakuna kitu kinaumiza kama watu kukudharau na kubeza uwepo wako si ndiyo? Dharau ina maana kwamba wanachukulia poa jambo au kitu fulani pasipo kukipa thamani inayostahili. Hivi unajua kwanini watu wanakudharau? Ukweli ni kwamba huwezi kuwa mwema na mzuri kwa kila mtu ila inakuwa inaumiza zaidi pale watu ambao umewapa nafasi kubwa kwenye maisha yako halafu wanakudharau. Inaumiza sana si ndiyo? Kuna baadhi ya sababu ambazo zinafanya watu wakudharau na ukiweza ku-deal nazo basi dharau zitatoweka na wataanza kukuthamani; 1. Furaha yako isiwategemee wao, Wanakudharau kwa sababu wanajua unawategemea wao ili uwe na furaha kwenye maisha yako, Anza sasa kujipa furaha wewe mwenyewe pasipo kuwategemea wao. 2. Umeruhusu watu kukuzoea kupita kiasi, Thamani ya kitu inakuwa kubwa kikiwa hakipatikani kirahisi, ishi nao vizuri ila weka mipaka ya kutoruhusu mazoea kupita kiasi “Mazoea yakizidi yanaleta dharau”- Lolo Facts. 3. Kuwa bize na maisha yako, Waingereza wanasema “Mind your own business” Kwahiyo acha kufuatilia maisha ya watu na kuwasema vibaya wakijua hilo watakudharau na kukuona ni mtu wa hovyo. Fanya yanayohusu muungwana. 4. .............. 5. .............. Hivyo basi... Mambo matano haya na uhakika yatakusaidia watu wasikudharau, kwa sababu unakuwa umejua nini ufanye ili uongeze thamani yako. Kujua mambo yote kwa urahisi na upana ni sehemu moja pekee ambayo ni MAISHA NI KUTHUBUTU PODCAST. Kwa sababu utaenda kujua kila kitu kwenye episode ambayo ina madini ya kuongeza thamani yako. Cha kufanya ni rahisi... Bofya link kwa bio kwa sasahivi Kusikiliza ujue sababu zinazofanya watu kudharau
…
continue reading
113 odcinków