COP29: Wanamazingira wapendekeza ufadhili zaidi kwa Afrika kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi
Manage episode 450969583 series 1146275
Mkutano wa hali ya hewa COP29 ukiendelea nchini Azerbaijan, masuala yanayoibua changamoto ni ufadhili, mchakato wa kuondokana na mafuta kisukuku, athari ambazo zimekumba bara la Afrika kutokana na mabadiliko ya tabia nchi, kuongezeka kwa viwango vya joto lakini pia suluhu zinazopendekezwa na wataalam wa mazingira.
Kauli mbiu ya mwaka huu kwenye mkutano wa COP29 ni uwajibikaji wa ufadhili haswa kutoka mataifa tajiri ambao wanachangia kwa viwango vikubwa uchafuzi wa mazingira wakati athari zake zinaathiri nchi zisizojiweza na shirika la mazingira la Greenpeace Africa linapendekeza mustakabali wa nishati mbadala na haki ya hali ya hewa kwa Afrika.
Kwa mengi zaidi bonyeza ili kusikiliza makala.
24 odcinków